Jumba la Nyaraka

Mkusanyiko wa Nyaraka za Kihistoria na Maktaba ya Vitabu vya Wamishenari

Kwenye hifadhi ya Nyaraka kuna Nyaraka muhimu za Kihistoria ambazo zilirekebishwa na kupangwa tena kiusalama zaidi ili zihifadhiwe. Utapata ufumbuzi mkubwa mno kuhusu Wamishenari pale utakaposoma shughuli zao kwenye Nyaraka za Kijerumani, Kidachi, Kiingereza, Kinyakyusa au Kiswahili. Ni safari ya kipekee itakayo kupeleka maeneo mbalimbali kama vile, Historia ya Misheni na Kanisa,Kutawazwa kwa Mchungaji wa kwanza wa Kitanzania 1932, Wafungwa wa Kimishenari wa Kijerumani kama Wafugwa wa Kivita 1940, Jumuiya ya Kimataifa ya Wamishenari baada ya Vita ya Pili ya Dunia, na muunganiko na mageuzi ya Kanisa la Moravian Africa katika kipindi cha kupigania Uhuru mwishoni mwa miaka ya 1960’s.

 

Historia na Mifano ya Nyaraka

 

Kwenye taarifa ya safari halisi, utakutana na Wamishenari wadogo ambao walisafiri toka Ulaya hadi Afrika Mashariki wakizungumza Kinyakyusa kwa msaada wa Kamusi ya Wamishenari wa Mwanzo, Au soma kichwa cha habari na ufungue kwenye maktaba yetu ya vitabu. Kwa msaada zaidi kuhusiana na Utafiti Binafsi au wa Kitaalam, Wasiliana na Mtunza Nyaraka

  • Categories

    • No categories
  • Archives

  • Meta