Jumba la Makumbusho

Mkusanyiko na Maonyesho ya Makumbusho

Mkusanyiko wa makumbusho ulianza rasmi mwaka 1991 na kupanuka zaidi mwaka 2007/2008, na unabeba na kuhifadhi vitu vya kihistoria kutoka wilaya za KMT-JK yaani Rungwe, Kyela na Ileje.

Katika maonyesho ya makumbusho vitu vinavyoonyeshwa hutueleza kuhusu mambo ya nyanja za maisha ya kimila, mambo ya tiba, ngoma za asili, uwindaji na mitindo ya mavazi, ya watu kutoka maeneo haya, wakiwemo Wanyakyusa na Wandali. Picha za kihistoria za kutoka katika mkusanyiko wa Jumba la Nyaraka na kuhifadhi nyanja mbalimbali za Kitamaduni, na hazioneshi katika uhalisia wake. Nyaraka hizi za thamani hutuonyesha pia jinsi Wamishenari wa Kimoravian na wenyeji walivyoshuhudia na kukabiliana na ulimwengu wa mabadiliko.

Watakaotembelea Maonyesho haya watapatakujua zaidi kuhusu Historia ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, Tanzania. Pia namna Wamishenari wa kwanza walipowasili Rungwe,kusambaa kwa kazi katika eneo hili, na maendeleo ya Kanisa mpaka hivi leo.

  • Categories

    • No categories
  • Archives

  • Meta