Mradi

Mazingira na Historia ya RAMC

Ili kupata ufahamu wa RAMC,haya ni maelezo ya mahali ilipo na historia yake Rungwe

Pindi Theophil Richard alipotembelea kwa mara ya kwanza eneo ambalo baadaye lilikuja kuwa kituo cha Wamishenari Rungwe. Kwenye kitabu chake alielezea hivi:

 

Freitag, den 21. August. Um 9 Uhr, mit drei Mann und dem Sonnenschirm auf Entdeckung, finden, dass wir in direkter Nähe ein Dorf von 100 Hütten haben, dass die Leute sehr fleissig sind, reich an Gärten, reich an Kühen, Mais, Pataten, Bohnen, Malesi (Hirse); Holz in der Nähe, die Stelle ist hoch genug gelegen, kein Dorf oberhalb am Wasser, gesund. Das Wasser ist schwer zugänglich, da es in einer tiefen Schlucht fliesst. Am Nachmittag neue Entdeckungstour, finden Lehm, Ton, zwei Quellen, die sich ableiten lassen und besseres Wasser liefern als der Fluss.“

(Richard 26)

“21, Ijumaa, Agosti, saa 3 kamili, nikiwa na watu watatu na mwamvuli wa jua tuligundua na kuona kijiji chenye vibanda 100, kiasi cha mita chache toka tulipo. Watu wake walikuwa wakifanya kazi kwa bidii, Utajiri wa Bustani, Ng’ombe, Mahindi Viazi, Maharagwe na Ulezi.Karibu kulikuwa na Kichaka, Eneo lilikuwa juu sana, hakukuwa na kijiji. Maji yalikuwa ni vigumu kuyafikia kwa sababu yalikuwa chini sana kwenye korongo refu. Wakati tunatembea mchana tuligundua chemchem mbili kwenye udongo Mfinyanzi. Ambapo tungeweza kutega bomba ili tupate maji mazuri kuliko yale ya mtoni.”

Jumba la Nyaraka na Makumbusho Rungwe

lililopo Rungwe, mkoani Mbeya. Kwenye Historia ya Kanisa la Moravian, Misheni ya Rungwe ni sehemu muhimu iliyoanzishwa mwaka 1891. Kanisa la Rungwe ndo la kwanza na lipo hadi hivi leo, Vilevile Makao Makuu ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini mwa Tanzania bado yapo hapa RAMC Kwenye Jubilei ya miaka 100 ya (KMKT) mwaka 1991, Mradi wa Jumba la Nyaraka na Makumbusho ulianzishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanisa Bwana. Angetile Musomba kwa lengo la Kukusanya, Kuunganisha na Kutunza (Vitu Nyaraka na Picha) za historia ya Kanisa la Moravian Tanzania Nyada za Juu Kusini na watu wanaopatikana Eneo hili.

Msaada toka Nje

Toka mwaka 2004-2006 kwa ufadhili wa kanisa la Moravian la Ujerumani limesaidi mradi huu msaada wa kifedha kwa ujenzi wa jengo jipya. Vilevile misheni 21 ya Uswisi ilchangia mradi huu kwa kutuma watu wane (4) waliochangia kuendeleza, kufanikisha na kusimamia ujenzi huu wa Jumba hili la Makumbusho na Nyaraka Rungwe. Tuliweza kukusanya vitu vya kipekee na vya ajabu karibu ya mamia ya vitu vya asili, Zaidi ya Mafaili 1000 yaliyokusanya nyaraka zisizohesabika toka mwaka1909 hadi leo hii na vitabu 700 vya Wamishenari ambavyo vilihifadhiwa, vilitunzwa na kukabidhiwa kwa KMT-JK.

Idara ya RAMC

Mwaka 2011 imejenga Idara ndani ya KMT-JK, na imekuwa ikiongozwa na kusimamiwa na Afisa wa Kanisa. Kwa ajili ya kuunganisha Idara hii na Taasisi nyingine na Jamii, Bodi ya Ushauri ilianzishwa ikikusanya mawazo mbalimbali kumsaidia Mtunza Nyaraka kuandaa na kufanya kazi ndani ya RAMC.

  • Categories

    • No categories
  • Archives

  • Meta